Korea Kaskazini yarusha Satelaiti yake ya kwanza


Na DW

NCHI ya Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kuweka satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi kwenye anga ya juu ya dunia Jumanne jioni na kuapa kusafirisha nyingine kadhaa katika muda mfupi ujao.



Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini KCNA, limesema kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un alishhuudia uzinduzi huo kutoka kituo kilichoko Tongchang-ri kwenye Pwani ya Magharibi ya nchi hiyo.

Roketi iliyotumika ya Chollima-1 ilisafiri kufuata njia ya kawaida iliyopangwa na kuiweka kwa usahihi satelaiti hiyo ya upelelezi Malligyong-1 kwenye mzunguko wake saa kadha baada ya kufyetuliwa angani, shirika la habari la KCNA liliripoti.

Maofisa wa Marekani na Korea Kusini hawajathibitisha hadharani iwapo satelaiti hiyo ilifika kwenye mzunguko wa anga ya juu ya dunia lakini wamelaani safari hiyo kuwa ni uchochezi unaokiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kufuatia hatua hiyo Korea Kusini imesitisha sehemu ya mkataba wa kijeshi iliyousaini Korea Kaskazini mwaka 2018, baada ya Pyongyang kupuuza tahadhari zilizotolewa na Marekani.

Hatua hiyo ya kusitisha kipengele katika makubaliano hayo, itashuhudia Korea Kusini ikiongeza doria za kijeshi katika mpaka wa nchi hizo.

Makubaliano hayo ambayo yamekuwa yananua kupunguza mivutano kati ya nchi hizo mbili yalisainiwa mwaka 2018 kati ya rais wa zamani wa Korea Kusini Moon Jae-in na Kim Jong Un

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *