Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza Viongozi, Majenerali, Maafisaa, Askari, Vijana, Watumishi na Wananchi mbalimbali katika Mbio za JKT Marathon Zilizofanyika leo Juni 25, 2023, Jijini Dodoma. Mbio hizo za Kilomita 5, 10 na 21 ziliazia na kutamatika kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Katika hotuba yake, Dkt Kikwete amepongeza Kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Pamoja na kumshukuru Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) kwa kumwalika ili awe Mgeni rasmi wa shughuli hiyo.
Dkt. Kikwete pia, amelitaka Jeshi, kupitia Wizara, lione uwezekano wa kufanya mbio za Marathon mara kwa mara Jijini Dodoma ili Wananchi waweze Kushiriki na kuimarisha afya zao.
Awali, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (Mb), amemshukuru na kumpongeza Dkt. Kikwete kwa kumuunga mkono Rais na Amri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anavyotoa hamasa kwenye Michezo nchini ikiwemo Jeshini.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Tulia Ackson Mwansasu, amepongeza kufaana kwa JKT Marathon 2023, aidha, alivutiwa na Kutoa zawadi kwa Mshiriki wa Mbio za Kilometa 5, aliyejitambulisha kwa Jina Mzee Mashaka, Kwa namna aliyokimbia na kumaliza ruti huku akiwahamasisha viongozi akiwemo Mgeni rasmi.
Nae, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda amesema Jeshi litaendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya michezo ndani na na nje ya Nchi.
Pamoja na mafanikio mengi kwa Wanamichezo Jeshini, Mkuu wa Majeshi pia ametumia fursa hio kuwapongeza TV Timu ya Jeshi ya Mashujaa fc, kwa kufuzu kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara, baada ya kuifunga Mbeya City fc kwa uwiano wa magoli 4 kwa 1 baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini.