Joshua amtandika Wallin kwa KO raundi ya tano

RIYADH, Saudi Arabia

Bondia Anthony Joshua, usiku wa kuamkia leo amemchapa Otto Wallin kwa KO katika raundi ya 5 huku hasimu wake Deontay Willder akipigwa kwa pointi na Joseph Parker.

AJ alikuwa katika kiwango bora kwenye pambano hilo lililofanyika Saudi Arabia na aliweza kuutawala mchezo kwa raundi zote tano za awali kiasi kwamba wasaidizi wa Wallin waliamua kurusha taulo mwisho wa raundi ya tano.

Ushindi huo, umepokelewa kwa furaha na mashabiki wa AJ lakini imekuwa pigo kwa mashabiki wa ngumi duniani kwa kukosa fursa ya kuona pambano kati ya bondia huyo dhidi ya Wilder.

Katika moja ya makubaliano ya mapambano hayo, ilikuwa ni kwamba kama Wilder na Joshua wote watashinda basi kulikuwa na fursa ya wawili hao kukutanishwa uliongoni mwaka 2024.

Hata hivyo kwasasa nafasi ya pambano hilo kutokea inaonekana kuwa finyu baada ya Wilder kupigwa.

Wilder alizidiwa kabisa maarifa na Parker ambaye alionekana kuutawala mchezo kwa muda wote wa pambano na hata alitangazwa mshindi kutokana na alama za majaji wote wa tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *