Jezi mpya Azam gumzo mitaani

Na Mwandishi Wetu

KLABU ya Azam FC, imezindua rasmi jezi zao mpya za msimu wa 2023/24 huku zikiwa gumzo mitaani kutokana na kuwavutia mashabiki wengi.

Uzinduzi huo ulifanyika Dar es Salam leo mchana huku timu yao ikiwa kambini nchini Tunisia ambapo juzi ilichapwa mabao 3-0 na Esperance de Tunis.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa klabu ya Azam, Tunga Ali amesema jezi hizo zimekidhi vigezo vyote vya ubora na zinadumu muda mrefu kwa zaidi ya miaka 10 bila kupauka.

Jezi ya nyumbani ni nyeupe, jezi ya bluu ni ya ugenini na jezi rangi ya dhahabu ni ya tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *