Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENKI ya I & MTanzania imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Pesapal Tanzania, kampuni yenye leseni ya huduma za malipo na suluhisho za kidigitali.
Kupitia ushirikiano huu, I&M Bank Tanzania itaongeza thamani kwa wateja wake wa kibiashara kwa kuwapatia huduma za mashine za Point of Sale (POS), mifumo ya biashara mtandaoni, pamoja na malipo kwa njia ya simu kwa masharti nafuu.
Ushirikiano huu unalenga kusaidia wafanyabiashara nchini Tanzania, hususan SME na kampuni za kati, kwa suluhisho salama, madhubuti, na yanayokua kwa ajili ya malipo ya madukani na mtandaoni.
Kwa pamoja, I&M Bank Tanzania na Pesapal wanahamasisha ubunifu wa kifedha na kusogeza huduma rahisi za kidigitali kwa wateja wa kibiashara.