LOS ANGELES, Marekani
MCHEZAJI wa mpira wa kikapu, James Harden, amepigwa faini ya dola 100,000 (zaidi ya sh. 250,500,000) na Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kwa kauli aliyoitoa kuwa hatoichezea timu yake ya Philadelphia 76ers kama Rais, Daryl Morey ataendelea kuiongoza timu hiyo.
Mlinzi huyo alimuita Morey muongo katika mahojiano baada ya taarifa kudai kuwa 76ers imesitisha mpango wa kumuuza.
Harden, 33, imeripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kujiunga na LA Clippers kabla ya mazungumzo kusitishwa.
NBA imeeleza faini hiyo imetokana na kauli yake aliyosema:”hatotoa huduma yoyote iliyomtaka chini ya mkataba wa mchezaji hadi pale atakapouzwa timu nyingine”.
Hata hivyo, Chama cha Wachezaji Kikapu cha Kitaifa, hakijaunga mkono kwa kusema: “Kwa heshima, hatukubaliani na uamuzi wa ligi wa kumwadhibu James Harden kwa maoni yake ya hivi majuzi, ambayo tunaamini hayakiuki sheria dhidi ya matakwa ya biashara ya umma.