Gigy Money: Fani ya urembo ina fursa

Na Mwandishi Wetu

BALOZI wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Winprincess ambaye pia ni Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford “Gigy Money”, ametembelea banda la Winprincess Casino akiwa na Washiriki wa Miss Tanzania katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba.

Akizungumza wakati alipotembelea banda hilo leo, Gigy Money, amesema kama Balozi ameona ubora wa Winprincess kutokana na kubashiri mechi mbali mbali na kushinda, huku akitoa wito kuweka fedha Winprincess kuliko kuweka fedha hizo kwenye kibubu.

Aidha, Gigy Money ameiomba Serikali iwaangalie warembo (Miss Tanzania) pia alishauri wazazi kuwapa vijana uhuru wa kuchagua fani hususani mabinti wanaopenda urembo kutokana na tasnia hiyo imefungua fursa nyingi kwa wasichana wadogo.

Pia ametoa mwito kwa vijana kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea kubashiri na Winprincess Casino kwani fedha zipo na yeye pia ni mmoja wa washindi wa kubashiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *