
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki, Tume ya Ushindani (FCC) inazuia makubaliano vanayofifisha ushindani baina ya washindani kwa upangaji bei usiofaa au kushusha bei kupita kiasi ili kuuwa ushindani.
Aidha, tume hiyo imesema inazuia matumizi mabaya ya nguvu ya soko ikiwamo vitendo vyote vinavyolenga kutumia nguvu ya soko kama kizuizi dhidi ya washiriki wengine na wapya katika biashara au huduma kwa kutumia mbinu kandamizi zinazolenga au kuwaengua au kuwadidimiza washindani katika biashara.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu maadhimisho ya siku ya Ushindani Duniani yatakayofanyika Desemba 5, mwaka huu.
Amesema pia wanadhibiti muungano wa kampuni unaofifisha ushindani ikiwamo kuhakikisha kampuni zinatoa huduma au kuzalisha mali zinatakiwa au zinahitajika kuitaarifu FCC kuhusiana na lengo la kuunganisha shughuli zao za kibiashara au kampuni moja kununua hisa za kampuni nyingine au kuinunua kampuni nyingine ili kuondoa ukiritimba unaoweza kutokea baada ya muungano huo. Kizingiti kilichowekwa na
Aidha, Ngasongwa amesema FCC kwa sasa thamani ya pamoja au mauzo ya mwaka yanayofikia Sh. bilioni 3.5 na kampuni ambazo zinapanga kuunganisha shughuli zao za kibiashara ambazo hazifikii thamani hiyo, zinaweza kufanya hivyo bila kulazimika kuitaarifu FCC.
“Tume ya Ushindani (FCC) itaadhimisha kitaifa Siku ya Ushindani Duniani mwaka 2025, Desemba 5, katika Hotel ya King Jada iliyopo Morrocco Square jjini Dar es Salaam ambapo Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Artificial Intelligence (AI), Consumers and Competition Policy iliyotafsiriwa kuwa “Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani”.”
Amesema maadhimisno hayo yameanza leo Desemba Mosi yataambatana na shughuli mbalimbali ikiwamo kutoa elimu na kuufahamisha umma kuhusu maadhimisho kupitia vyombo vya habari, semina kwa Mamlaka za Udhibiti, semina kwa wanasheria mbalimbali na kufanya kongamano maalum la Siku ya Ushindani Duniani.
“Shughuli tajwa hapo juu zitahuishwa na kauli mbiu ya mwaka huu “Artificial Intelligence (Al), Consumersand Competition Policy inayotafsiriwa kuwa,” Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani”.
“Kauli mbiu ya mwaka huu imekuja katika wakati muafaka ambapo pamoja na mambo mengine Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa akisitiza matumizi ya TEHEMA na Mifumo katika ufanyaji kazi pamoja na kuwahudumia wadau wetu.
Teknolojia, matumizi ya TEHAMA na Mifumo ikiwamo matumizi ya Akili Mnemba inakuwa kwa kasi sana na hivyo basi FCC haina budi kuhakikisha inaangalia vizuri matumizi ya Akili Mnemba katika kusimamia soko la ushindani nchini,” amesema Ngasongwa.