Evans atwaa ubingwa Citi Open

WASHINGTON DC, Marekani

MUINGEREZA namba mbili kwa ubora ndani ya taifa hilo, Dan Evans, ametwaa taji kubwa la kwanza katika maisha yake ya mchezo wa tenisi baada ya kumfunga Mholanzi, Tallon Griekspoor katika fainali ya michuano ya Citi Open jijini hapa.

Nyota huyo, 33, alipata ushindi huo licha ya kuwa na vikwazo vya mvua na kutwaa taji lake la kwanza la ATP 500 ikiwa ni la pili kwa upande wa Tour, akishinda kwa seti 7-5 6-3.

Seti ya kwanza ilionekana kuwa kwa Griekspoor, ambaye alikuwa akiwania taji lake la tatu msimu huu, alipiga mipira miwili aliyopata pointi kuelekea mchezo wa nne.

Evans ambaye kwa ubora wa viwango vya Dunia ni wa 40, aliongoza kwa seti 5-4, na kisha alibadili raketi yake katika mchezo uliofuata baada ya kuvunja mkono wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *