DMI kubadilishana uzoefu na Chuo cha Italia

Na Mwandishi Wetu, Italy

CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Chuo cha Italian Shipping Academy kilichopo nchini Italia.

Hati hizo ni za kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu.

Makubaliano hayo yamesainiwa nchini Italy na Dkt. Tumaini Gurumo, Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy (FAIMM) Eugenio Massolo.

Kwa upande wake, Mkuu wa chuo cha DMI, Dkt. Gurumo alisema kuwa makubalino hayo ya miaka mitano yatasaidia kuongeza ujuzi kati ya wanafunzi na Wahadhiri kwa pande zote mbili.

“Nimefurahi sana kuingia makubaliano haya kwa kuwa wenzetu wapo tayari kushirikiana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia,” alisema.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mahmoud Thabit Kombo, alisema Italy imepiga hatua katika teknolojia hivyo utayari wao wa kushirikiana na DMI utaiwezesha zaidi Tanzania kukua katika eneo hilo.

Alitoa wito kwa pande zote mbili kuteleza vipengele vya makubaliano ipasavyo ili izae matunda yanayotarajiwa.

Mkuu wa Chuo cha Italian Shipping Academy Foundation (FAIMM), Massolo alisema makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi Tanzania nchini Ital, Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania, Marco Lombardi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *