Dkt. Samia kutoa zawadi ya barabara, taa Buhigwe

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

MGOMBEA Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kutandaza mtandao wa barabara za lami na taa za barabarani katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, ikiwa ni zawadi yake binafsi kwa wananchi wa eneo hilo.

Hatua yake ya kutoa zawadi hiyo, amesema inatokana na Buhigwe kuwa chimbuko la Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt Philip Mpango, ameyesema amemsaidia vema kazi za ujenzi wa nchi.

Hii ni zawadi ya pili inaahidiwa na Dkt. Samia katika kampeni zake za urais, baada ya awali, kuwaahidi wananchi wa Mbeya kuwawekea taa za barabarani, baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchi.

Dkt. Samia ameyasema hayo leo, Jumamosi Septemba 13, 2025, alipozungumza na wananchi wa Buhigwe mkoani Kigoma, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Ameahidi kuongeza mtandao wa barabara za lami wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, sambamba na taa za barabarani, ikiwa ni zawadi ya Serikali kwa wakazi wa eneo hilo ambalo ni chimbuko la Makamu wa Rais, Dkt Mpango.

“Buhigwe ni Wilaya kubwa, imetoa mtu mkubwa. Sina wasiwasi na wilaya hii na CCM, sina wasiwasi. Kwa hiyo sasa ni heshima kwa sisi kuja mbele yenu hapa mimi mgombea urais, mgombea ubunge na udiwani,” anasema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *