LONDON, England
NYOTA wa mchezo wa tenisi, Novak Djokovic, ametuma ujumbe kwa wapinzani wake wanaowania Grand Slam baada ya kumchapa Andrey Rublev na kutinga nusu fainali ya michuano ya Wimbledon, akisema hilo halitokea.
Djokovic ambaye ni raia wa Serbia, alishinda kwa seti 4-6 6-1 6-4 6-3 uwanjani Centre Court na kumpeleka hatua ya nne bora ya mashindano makubwa kwa mara ya 46, akifikia rekodi ya Roger Federer ya muda wote kwa upande wa wanaume na pia kuongeza idadi ya meshi alizoshinda katika michuano hiyo kwa kufikia 33.
Djokovic anatakiwa kushinda mechi mbili ili kutwaa Grand Slam yake ya 24, ingawaje hadi sasa hajaonesha kiwango kizuri, hivyo utakuwa mtihani mwingine kumzuia nyota huyo, 36 kutwaa taji lake la nane la michuano hiyo.
Alipoulizwa anajisikiaje kiala siku anakuwa ni mtu wa kuwindwa, Djokovic amesema: “Napenda hilo. Kila mchezaji wa tenisi anapenda kuwa katika nafasi ambayo kila mmoja atataka kushinda dhidi yako.
“Shinikizo ni fursa, kama alivyosema Billie Jean King. Kamwe haitoondoka.
“Huamsha hisia nzuri zaidi ndani yangu na hunitia motisha zaidi ya yale ambayo nimewahi kuota na kunitia moyo kucheza tenisi yangu bora zaidi.
“Najua wanataka kupata ngozi ya kichwa changu, wanataka kushinda, lakini haitotokea.”
Rublev alicheza mechi nzuri lakini akaambulia kipigo tu kwa Djokovic, huku Mrusi huyo akiwa mchezaji wa kwanza katika enzi hizi kupoteza mechi nane za kwanza za robo fainali ya Slam.
Ciao…