Diamond aanza na ‘My Baby’

Na Mwandishi Wetu

MSANII wa muziki wa Bongofleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, ametimiza ahadi yake kwa mashabiki wa muziki baada ya kuachia wimbo mpya mapema jana.

Siku za hivi karibuni msanii huyo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Intagram kuanzia Julai Mosi, mwaka huu atakuwa akiachia ngoma kali bila kituo hadi mwakani.

Msanii huyo ambaye ni mmliki wa lebo ya muziki ya Wasafi, alisema kwakuwa Julai ni mwezi wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama yake, basi atakuwa akitesa katika soko la muziki hadi mwakani ambapo atampisha msanii mpya anayetarajiwa kutambulishwa kwenye lebo hiyo.

Diamond jana aliachia video ya wimbo mpya ujulikanao kama ‘My Baby’, aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria, Chike Ezekpeazu Osebuka ‘Chike’.

Ciao…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *