- Kibao chake cha ‘Gangsta’s Paradise’ kilibadili ulimwengu wa hip-hop
Na Mashirika ya Habari
KIFO cha rapa aliyeshinda Tuzo ya Grammy nchini Marekani Coolio mnamo Septemba 2022 kilitokana na athari za fentanyl na dawa zingine, meneja wake alisema.
Jarez Posey alisema familia ya mwanamuziki huyo ilikuwa imefahamishwa kuhusu matokeo hayo na daktari wa maiti wa Kaunti ya Los Angeles.
Msanii huyo alikutwa amepoteza fahamu katika sakafu ya bafuni ya nyumba ya rafiki yake miezi sita iliyopita. Alikuwa na umri wa miaka 59.
Coolio, ambaye jina lake halisi lilikuwa Artis Leon Ivey Jr, alishinda Tuzo ya Grammy kwa wimbo wa mwaka 1995 wa Gangsta’s Paradise.
Wimbo huo – ambao baadaye ulichaguliwa kama wimbo wa sauti wa filamu ya Dangerous Minds – uliendelea kuwa mojawapo ya nyimbo za rap zilizofanikiwa zaidi wakati wote ukiuza nakala zaidi ya milioni sita.
Unaendelea kusikilizwa na watu wengi na umesambazwa mara bilioni moja kwenye YouTube.
Wakati wa kifo chake, rapa huyo alikuwa akiugua ugonjwa wa moyo na pumu, mshirika wa BBC wa Marekani CBS News anaripoti.
Ingawa Coolio alikuwa ametumia hivi karibuni dawa aina ya phencyclidine, au PCP hivi majuzi, kifo chake kilitokana na athari za mlo wa fentanyl, heroini na methamphetamines, CBS ilisema.
Ofisi ya mchunguzi wa maiti iliona kifo chake kuwa bahati mbaya.
Coolio alianza kufanya muziki katika miaka ya 80, lakini aliimarisha nafasi yake katika historia ya hip-hop aliporekodi wimbo wa Gangsta’s Paradise.
Aleta mapinduzi ya hip-hop
Coolio aliposikia sauti ya wimbo uliokuja kuwa Gangsta’s Paradise, alikuwa na maoni sawa na sisi wengine.
“Nilihisi, ‘wow, napenda sana wimbo huu.’”
Rapa huyo – mzaliwa wa Pennsylvania na kukulia huko Compton, Los Angeles – alikuwa nyumbani kwa meneja wake mnamo 1995 kuchukua hundi, alipomwona mtayarishaji Doug Rasheed akijaribu kuuandaa wimbo huo kwenye chumba kingine.
“Kwa hiyo nikamwambia Doug, ‘Hey! Hii ni nini?’
“Alisema, ‘Ni wimbo tu tunafanyia kazi.’
“Na mara moja nikasema, ‘Ni wangu.’
“Niliboresha mstari mzima wa kwanza, kisha nikaketi na kuchukua kalamu na kuanza kuandika.”
Wimbo huo ulitolewa mnamo Agosti 1995 na, ukichochewa na video ya kukumbukwa iliyomshirikisha Michelle Pfieffer, uligonga vichwa vya habari.
Ukishirikisha Kwaya ya Malaika (ambayo aliimba yeye mwenyewe), pamoja na hadithi ya chapa ya biashara ya Coolio, ulikifanya kibao hicho kuvuma hewani papo hapo.
Ulikuwa wimbo wa kwanza “mzito” wa Rap kuingia katika chati za Uingereza na Marekani, ukifungua njia kwa wasanii kama 2Pac na Notorious BIG, ambao, hadi wakati huo, walikuwa wamechukuliwa kuwa wabaya sana kwa muziki maarufu.
Na umaarufu wake haukupungua. Wimbo uliouzwa zaidi mwaka 1995 nchini Marekani, Gangsta’s Paradise, una mitiririko zaidi ya bilioni 1 kwenye mitandao ya Spotify na YouTube.
“Nilifikiri itakuwa rekodi itakayochangamsha maeneo jirani,” Coolio aliiambia The Voice 2017. “Sikuwahi kufikiria kuwa ingefikia ukubwa uliofikia: umri wote, rangi, jinsia, nchi na vizazi.”
Bado, Gangsta’s Paradise ulilazimika kukabili vizuizi kadhaa kabla ya kufika ulipofikia.
Mvulana kutoka Compton…
Coolio alizaliwa na kupewa jina Artis Leon Ivey, huko Pennsylvania, na kuhamia hadi Compton akiwa mtoto, kitongoji maskini cha Waafirika wa kusini mwa Marekani, mjini Los Angeles. Alikuwa akisumbuliwa na pumu ya muda mrefu, alikuwa mwandishi wa vitabu na alifaulu katika masomo yake.
“Niliishi katika maktaba hiyo,” aliliambia jarida la Rolling Stone wakati wa ziara ya maeneo aliyoshi utotoni mwaka 1995.
“Nilisoma vitabu vyote vya watoto walivyokuwa navyo.”
Mambo yalianza kubadilika wazazi wake walipotalikiana baada ya kufikisha miaka 11.
Akitafuta kuingiliana na ulimwengu, alianguka katika maisha ya genge na kuishia kuwa picha ya kutisha, mitaani.
Miaka michache baadaye, alikamatwa kwa kuwa na bunduki shuleni. Kabla ya kufikisha miaka 20, alikuwa ametumikia kifungo kwa wizi.
Muziki wa hip-hop
Coolio baadaye alisomea katika Chuo cha Jamii cha Compton, ambapo aligundua kipaji chake cha uimbaji. Chini ya jina lake jipya la kisanii – Coolio Iglesias, akimwiga mwimbaji Julio Iglesias – alitoa nyimbo chache mtaani, lakini matumizi mabaya ya dawa za kulevya yaliharibu kazi yake.
Akiwa na umri wa miaka 20, alihamia San José ili kuishi na baba yake, huku akifanya kazi ya kuzima moto; na baadaye akausifu Ukristo kwa kumsaidia kushinda uraibu wake wa dawa za kulevya.
Albamu yake ya kwanza, It Takes a Thief, ilirekodiwa mwaka 1994 na ilisifiwa kwa mchanganyiko wake wa midundo ya kufurahisha na mashairi ya kijamii.
“Walinzi” wa hip-hop hawakupendezwa na udhanifu kama huo. Msimamo wa kupinga unyanyasaji na kukubalika kwa namna fulani ulifanya ionekane “laini”.
Lakini ukaja wimbo wa Gangsta’s Paradise.
Muziki mzuri
Siku moja, Doug Rasheed alitoa nakala yake ya albamu mbili za Stevie Wonder za mwaka 1976, Songs In The Key Of Life na kuchukua sampuli ya wimbo wa Pastime Paradise, wimbo wa huzuni, ambao ulikuwa mojawapo ya nyimbo za kwanza kuchukua nafasi ya orchestra.
Rasheed aliongeza mdundo mkali na bezi ya kutisha, kisha akapeleka wimbo huo kwa mwimbaji Larry “LV” Sanders, ambaye alitoa sauti ya kuongezea kibao hicho na kuimba kiitikio.
“Nilikuja nikiimba ‘Pastime Paradise,’ lakini nikabadilisha kuwa ‘Gangsta’s Paradise,’” aliiambia Rolling Stone kuhusu hadithi ya wimbo huo mnamo mwaka 2015.
“Niliimba sehemu zangu, sauti zote, na nilifanya kwaya. Kwaya hiyo yote unayosikia ilikuwa mimi, nilifanya sauto zote, kutoka soprano, tenor hadi bezi.”
LV Sanders alitaka rapa aonekane kwenye wimbo huo na akampa rafiki yake Prodeje, ambaye alikataa. Kisha Coolio akamsikia. Akiwa amekasirika, alianza kuandika mashairi mara moja.
Barua
Maneno ya ufunguzi, yenye kutegemea Zaburi ya 23, yalikuja akilini papo hapo: “Ninapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti/nayatazama maisha yangu na kugundua kwamba bado hakuna mengi,” kisha nikaketi na kushika kalamu na kuanza kuandika,” alikiambia kipindi cha YouTube Hot Ones mnamo mwaka 2016.
“Ilikuwa wimbo wa kumuomba Mungu’’.
Coolio alikuwa na umri wa miaka 30 wakati wimbo huo ulipoandikwa, lakini msimulizi ana umri wa miaka 23 na hajui kama ataweza kufikisha 24. “Alilelewa mitaani”, amezama katika maisha ya uhalifu na kulipiza kisasi. Mtu akivuka, ataishia “chaki”.
Lakini hadithi hiyo haitukuzi kamwe maisha ya majambazi. Msimulizi huomba kila usiku, akijua kwamba amenaswa. Katika mstari wa mwisho, anashutumu serikali kwa kumtupa.
“Wanasema lazima nijifunze, lakini hakuna mtu hapa wa kunifundisha/Ikiwa hawawezi kuelewa, wanawezaje kunifikia?”
Zaidi ya kazi yake iliyochukua miongo minne alirekodi albamu nane za studio na akashinda Tuzo la Muziki ya Amerika na Tuzo tatu za Muziki za Video za MTV.
Vibao vyake vingine ni pamoja na C U When U Get There, Fantastic Voyage, Rollin’ With My Homies, 1, 2, 3, 4 (Sumpin’ New), na Too Hot.
Coolio, ambaye hakuacha wosia, alikuwa na watoto 10, wakiwemo wanne aliozaa na mkewe Josefa Salinas, ambaye walioana mwaka 1996 na kuachana mwaka 2000.
Mnamo Machi 2022, aliliambia jarida la Today Extra la Australia kwamba alikuwa na wajukuu watano.
Coolio alikuwa mgombea mwenza wa urais wa mcheza filamu za utupu mwanamama Cherie DeVille kupitia Chama cha Democratic mwaka 2020 kabla ya mwanamama huyo hajajitoa.