Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amesema kwamba tatizo la udumavu katika Wilaya Mufundi bado ni kubwa licha ya wilaya hiyo kuwa wazalishaji
Akizungumza na Wazee, viongozi wa dini pamoja viongozi mbalimbali wa Chama hicho wilayani Mafinga mkoani Iringa , Chongolo amesema iko haja ya kuhamasisha ulaji wa chakula bora ili kuondoa udumavu kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Amesema kwamba bila kufanya hivyo ni vigumu kupata wazalishaji mali wenye akili timamu watakaosaidia maendeleo y mufindi huku akiwakumbusha viongozi hao kuendelea kutoa elimu kuhusi maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuwa mufindi takwimu zinaonyesha bado maambukizi yako juu.
“Ni wajibu wa viongozi kutoa elmu kwa wananchi ili kupunguza idadi ya watu wanaoambukizwa vvu, ” amesema Chongolo ambaye yupo kwenye mkoa huo kwa ziara yake ya siku saba ya kuimarisha uhai wa chama kuanzia ngazi na shina pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020‐ 2025.