KLABU ya Simba, imemtambulisha beki wa kati, Che Fondoh Malone Junior, kuwa mchezaji wake mpya kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Coton Sport ya kwao, Cameroon ikiwa ni siku chache tangu wamtoe Joash Onyango kwa mkopo kwenda Singida Fountain Gate.
Che Malone,24, anakuwa mchezaji mpya wa tatu wa Simba SC baada ya winga wa kushoto, Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast na mshambuliaji Mcameroon, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
Malone anatua Msimbazi baada ya kuisaidia Coton kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Cameroon huku yeye mwenyewe akishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa 2022-2023.