Na Sarah Moses, Dodoma.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Mary Chatanda amewataka wagombea waliochaguliwa kuwania nafasi za Ubunge Vitimaalum kufanya kampeni ili kuhakikisha chama kinapata kura zakutosha zitakazowezesha nafasi za viti maalum kuwa nyingi.
Pia amesema Mkutano Mkuu Maalum wa UWT unatarajia kufanyika kesho ambapo Wajumbe zaidi ya 1000 watashiriki kupiga kura kuchagua Wabunge makundi maalum
Hayo ameyasema leo Julai 1,2025 jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema maandalizi yote yamkutano yameshakamilika huku akiwaalika Wajumbe wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuhudhuria mkutano huo.
Amesema kuwa waliochaguliwa siyo kwamba wamepita mojakwamoja bali kinyanganyiro kinaendelea hivyo wanapaswa kufanya kampeni ili kuhakikisha chama kinapata kura za kutosha zitakazowezesha nafasi za viti maalum kuwa nyingi.
“”Ushindi wa kura siyo uteuzi bado kuna Vikao vingine ambavyo vitaendelea kuchuja mpaka pale chama kitakapo toa mtu wakwenda kutafuta kura” amesema.
Vilevile amesema kuwa kila baada ya miaka 5 UWT hufanya uchaguzi wa viongozi wa serikali nakuongeza kuwa mkutano huo utahusisha upigajikura kwa makundi maalum 4.
“Makundi hayo ni pamoja na Asasi za Kiraia, Wasomi wa Vyuo Vikuu, Wafanyakazi pamoja na Watu wenye ulemavu” amesema.
Amesema kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu imeteua wagombea 8 kwenye kila kundi huku akiwaaasa Wajumbe kupiga kura kwa watu wanaowapenda wao nasiyo aliyewapa kitu.
“Wakachague viongozi kwa haki na siyo waliotoa rushwa kwani chama chetu kumeshaelekeza nakupiga vi ya rushwa.
” Tunaelewa wagombea wamekuja na wapambe wao hivyo basi Wajumbe wanatakiwa kuwa makini”amesema Chatanda.
Katika hatua nyingine Chatanda amewasisitiza wagombea watakao chaguliwa kuwania nafasi hizo wasibweteke kwani bado safari ni ndefu yakuweza kuchaguliwa .
“Ushindi wa kura siyo uteuzi bado kuna Vikuu vingine ambavyo vitaendelea kuchuja hivyo waendelee kuomba kura .
Mwisho.