Chasambi rasmi atua Msimbazi

Na Badrudin Yahaya

KLABU ya Simba, imetangaza kukamilisha usajili wa Winga, Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Mchezaji huyo alipandishwa na Mtibwa Sugar msimu huu kutoka timu ya vijana na amefunga bao moja huku akitengeneza mengine mawili.

Chasambi ambaye mara kadhaa amejumuishwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ msimu huu, anaungana na nyota wengine wapya wa Simba ambao walitambulishwa awali, Saleh Karabaka na Babacar Sarr chini ya Kocha, Abdelhak Benchikha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *