Benki ya Equity,PASS na MCODE zasaini mkataba kuwakomboa wakulima

Na Sarah Moses, Dodoma.

BENKI ya Equity imeingia mkataba na taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) na Movement for Communite Development (MCODE) kwaajili ya kuboresha maisha ya Mtanzania na hasa wakulima wadogo wadogo ambao wapo vijijini na walitaka kupata huduma za kifedha hususani mikopo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Agosti 5,2024  Meneja Mkuu wa Biashara wa Benki ya Equity Leah Ayoub mara baada ya kusaini mkataba huo ulioshuhudiwa na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde katika viwanja vya maonesho ya Nanenane vilivyopo Nzuguni Jijini Dodoma amesema kuwa lengo lao hasa kama Equity ni kuboresha maisha ya mtanzania akiwemo mkulima

Amesema wamekuwa wakipata changamoto yakupata dhamana hivyo PASS wameungana na Equity ili kuwaunga mkono wakulima wadogowadogo waweze kupata dhamana ya mkopo bila gharama yoyote na hivyo gharama hiyo wao kama benki wanaichukua.

“ Wakulima wao wanadhaminiwa hadi asilimia 80 ya dhamana ambayo itakuwa imepelea wakati anapokuwa anachukua mkopo’amesema.

Pia amesema PASS na MCODE itaendelea kushirikiana na MCODE katika kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo ,lakini pia watatoa mikopo mikubwa kwa wajasiliamali wakubwa mpaka wajasiliamali wadogo huku akiongeza kuwa mikopo hiyo itakuwa ikitolewa kwa wakulima ambao wanajihusisha na kilimo cha mahindi mkoani Ruvuma ,na mikoa mingine ambayo ipo nyanda za juu.

“Tutatoa mafunzo kwa hawa wakulima jinsi ya kutumia mikopo hiyo kwa usahihi ili waweze kulipa mikopo yao na pia wataendelea kutoa mikopo ambayo itakuwa na gharama ya bei nafuu ambayo haitamuumiza mkulima pale anapovuna ataweza kulipa mkopo lakini atabaki na faida’amesema.

Amesema lengo lao hasa kama Equity ni kuboresha maisha ya mtanzania ,yamkulima na kubadilisha hatima ya mkulima mdogo ili aweze kukuwa na kuwa mkulima mkubwa ambaye anaweza akajitegemea akawa na trekta akaweza pia kuchakata yale mazao ambayo anayavuna.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Biashara kutoka Private Agricultural Sector Support (PASS) Adam kamanda amesema mkataba walioingia na Equity benki ni kwaajili ya uenderevu kibiashara ambapo wao wametoa  dhamana na benki ikatoa fedha kwaajili ya kuwasaidia  wakulima kuweza kupata viuatilifu,mbegu,madawa na kulima kisasa ili kuongeza tija katika mazao yao.

“Tunategemea hawa watu 30,000 ambao tulianza nao waende zaidi ili hata wafike watu laki moja tutaendelea kufanya hivi nchi nzima”amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Movement for Communite Development (MCODE) Slaiton Godfrey amesema kuwa wamefanikiwa kupata mikopo kupitia wakulima wao kiasi cha shilingi bil.20 ambapo kwa sasa wanavikundi zaidi ya 1000 kwenye mikoa 6.

“Tulikuwa tumejikita katika mahindi peke yake lakini kwa sasa kwa na msimu ujao wamejikita pia kwenye Mpunga na Viazi lakini pia wanategemea kuingia katika zao la Avocado .

MWISHO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *