Barca kutoa nyota watatu, fedha kwa Mbappe

CATALUNYA, Hispania

KLABU ya Barcelona, imeripotiwa kuwa tayari kutoa ofa ya wachezaji watatu na fedha kwa PSG ili kubadilishana na straika wao, Kylian Mbappe.

Miongoni mwa nyota hao ni Ousmane Dembele, ambaye tayari ameshakubali mkataba wa miaka mitano kujiunga na miamba hiyo ya Ligue 1.

Mbappe, 24, anaonekana yupo njiani kuondoka PSG kipindi hiki baada ya kuingia mwaka wa mwisho katika mkataba wake.

Straika huyo anaonekana atasajiliwa akiwa mchezaji huru na Real Madri katika dirisha lijalo la usajili.

Lakini PSG ilikubalikumuuza mwezi huu, kutokana na ofa iliyowekwa mezani ya pauni milioni 259 kutoka Saudi Arabia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *