Azarenka azomewa kutolewa Wimbledon

LONDON, England

MCHEZAJI tenisi wa kimataifa wa Belarus, Victoria Azarenka, amesema si uungwana kuzomewa na mashabiki akiwa anatoka uwanjani wakati wa michuano ya Wimbledon baada ya kufungwa na Elina Svitolina wa Ukraine.

Svitolina hakushikana mikono na warusi au mbelarusia baada ya mchezo tangu vita ya Ukraine ilipoanza.

Amekuwa akiweka wazi suala hilo tangu mwanzo, hata kabla ya kukutana na Azarenka uwanjani, walikuwa ni mashabiki wa Belarusia ndio waliozomea wakati akitoka uwanjani.

“Nini nimefanya? Nikae na kusubiria?” amesema Azarenka alipowauliza waandishi wa habari.

“Hakutaka kushikana mikono na watu wa Urusi, wala Belarus. Naheshimu uamuzi wake.”

Mbele ya mashabiki waliokuwa wakifuatilia mashindano hayo, Svitolina aliyeingia kama mwalikwa, alisha kwa seti 2-6 6-4 7-6 (11-9) na kutinga robo fainali.

Baada ya mechi ya kwanza Svitolina kupata pointi, Azarenka alionesha kumpungia mkono kwa kumpa heshima hata hivyo nyota huyo wa Ukraine hakuonesha kujali.

Badala yake zilisikika kelele za kumzomea wakati Azarenka, 33 akitoka uwanjani bila kuonesha ishara yoyote kwa mashabiki.

Ciao…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *