Azam FC yashusha straika la Colombia

Na Badrudin Yahaya

KLABU ya Azam FC, imekamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Colombia, Franklin Navarro ambaye alikuwa anacheza timu ya Cartulua.

Usajili huo ni wa kwanza kutangaza kwa vinara hao wa Ligi Kuu Bara katika dirisha hili la usajili.

Mshambuliaji huyo kabla hajatambulishwa na Azam alikuwa akihusishwa pia kujiunga na timu ya Simba.

Kwasasa kikosi cha Azam kipo katika michuano ya Mapinduzi Cup visiwani Zanzibar na wameanza kwa suluhu katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Mlandege.

Azam ambao ndio mabingwa mara nyingi zaidi wa michuano hiyo, ilipanga kikosi chenye nyota mchanganyiko wakiwemo wachezaji wao tegemeo Prince Dude, Allasane Diao, Yannick Bangala, Edward Manyama, Ayoub Lyanga na James Akaminko.

Hata hivyo, licha ya kuwa na nyota wote hao uwanjani lakini Mlandege walionekana kuwa sehemu nzuri zaidi ya kuibuka na ushindi ila walikosa umakini.

Azam watashuka tena dimba Desemba 30 kucheza na Chipukizi wakati huo Mlandege wao watakabiliana na Vital’O ya Burundi siku hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *