Na Zahoro Mlanzi
KATIKA kuhakikisha inatoa ushindani katika Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa, Klabu ya Azam, imemsajili straika wa kimataifa wa Senegal, Alassane Diao aliyekuwa akikipiga US Goree ya nchini kwao.
Huo unakuwa ni usajili wa tatu kwa miamba hiyo yenye maskani yake Chamazi kufanya, ikiwa imeshawasajili Feisal Salum na Gibril Sillah aliyesajiliwa kutoka Raja Athletics ya Morocco.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika mtandao wa klabu hiyo, iliandika:“Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji hatari Alassane Diao.”
Nyota huyo amesajiliwa na klabu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kumalizika mkataba wake Juni 30, mwaka huu sawa na mchezaji mwenzake, Samba Seck.