AUWSA kutekeleza miradi ya bilioni 4.2

Na Sarah Moses, Dodoma.

KATIKA bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazigira Jiji la Arusha (AUWSA) imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali za kuboresha huduma za majisafi na uondoaji wa majitaka kwa wakazi wa Jiji la Arusha zitakazogharimu jumla ya shilingi bilioni 4.2.

Hayo ameyasema Machi 14 ,2025 jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Justine Rujomba kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita amesema kupitia Mradi mkubwa, AUWSA imefanikisha upatikanaji wa majisafi kwa asilimia 99.

Ametaja shughuli zitakazofanyika kuwa ni pamoja na kutekeleza mradi wa maji Shangarai, kukamilisha utekelezaji wa mradi wa maji Kiranyi-Ngateu, kupanua mtandao wa majisafi urefu wa kilomita 76 ili kuunganisha wateja 14,000 kwa mwaka pamoja na kuhamisha dira za wateja 2,370 na kuziweka karibu na makazi ya watu.

Shughuli nyingine ni kuboresha na kuongeza mtandao wa majitaka kwa fedha za ndani kwa km 10, kuongeza wateja 1,000 wa majitaka, kuanza ujenzi wa ofisi mpya ya Kanda ya Monduli ili kuboresha mazingira ya kutolea huduma kwa wananchi na kuboresha mtandao chakavu wa majisafi katika maeneo mbalimbali hasa katika miji midogo.

“AUWSA imejipanga kutekeleza miradi na kutoa huduma kwa ufanisi ili kuhakikisha wananchi wa Arusha wanapata majisafi, salama na ya kutosheleza. Mamlaka itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali ili kufanikisha adhma ya kuhakikisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira zinaboreshwa kwa maendeleo endelevu ya Jiji la Arusha na maeneo ya pembezoni”, amesema

Vilevile amesema masaa ya upatikanaji wa huduma ya maji yameongezeka kutoka saa 16 (2020/21) hadi saa 22 mwaka 2024/25, pia idadi ya wateja waliounganishwa na huduma za maji imeongezeka kutoka 71,183 (Juni 2021) hadi 134,000 hadi kwa sasa.

Katika hatua nyingine amesema  bajeti ya mwaka wa fedha 2024/252025/2026, AUWSA imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali zitakazogharimu kiasi cha  bilioni 11.874.2, ili kuimarisha huduma.

 Shughuli hizo ni pamoja na Kujenga mtandao mpya wa maji safi wa km 215.96, Kuunganisha wateja wapya 13,993 ,Kuongeza mtandao wa majitaka kwa km 10, Kuunganisha wateja 4,200 kwenye huduma ya majitaka Kuboresha mtandao chakavu wa maji safi kwa km 64, Kutunza na kuboresha vyanzo vya maji na matanki ya kuhifadhi majiKutekeleza mradi wa maji Shangarai

“Kukamilisha utekelezaji wa mradi wa maji Kiranyi-Ngateu (Kulaza kilomita 3 za bomba),Kupanua mtandao wa majisafi urefu wa kilomita 76 (Kati (9), Lemara (2.5), Moshono (10), Murieti (15), Safari City (8), Ngaramtoni (9), Longido(4), Monduli (5.5), Mirerani (8) na Usa River (5),)) ili kuunganisha wateja 14,000 kwa mwaka” amesema

Pamoja na hayo, Mhandisi Rujomba ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ndani ya kipindi cha miaka minne imeleta mageuzi makubwa katika sekta ya maji ambayo yamekuwa na athari chanya hususani kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *