MARSEILLE, Ufaransa
STRAIKA Pierre-Emerick Aubameyang, imeripotiwa amekubaliana kila kitu kujiunga na miamba ya Ligue 1, Marseille.
Nyota huyo amekuwa hana msimu mzuri ndani ya Chelsea na anatarajia kuondoka ndani ya klabu hiyo kipindi hiki.
Amecheza katika mechi 15 za Ligi Kuu England akiwa na timu hiyo tangu alivyojiunga nayo mwaka jana, amefunga bao moja.
Inaelezwa amekubali kusaini mkataba wa miaka mitatu na Marseille, kwa mujibu wa mtandao wa Fabrizio Romano.
Chelsea nia ya kutaka kumuuza na hiyo ina maana imekubali moja kwa moja ada ya uhamisho ambayo imeripotiwa.
Mashabiki wa Arsenal, waliwakejeli kuhusu uhamisho huo na kuitaja Marseille imekuwa nyumba ya wastaafu kwa wachezaji wa zamani wa Arsenal kama ilivyokuwa kwa Alexis Sanchez na Matteo Guendouzi.