RIO DE JANIERO, Brazil
KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, atakuwa kocha wa timu ya Taifa ya Brazil mwakani.
Ancelotti, 64, ambaye ni raia wa Italia, ataendelea kuwa kocha wa miamba hiyo ya Hispania hadi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu wa 2023/24.
Kisha atakapokwenda kuinoa Brazil katika michuano ya Copa America msimu ujao ambayo itakayofanyikia Marekani.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Brazil, Ednaldo Rodrigue, amethibitisha mpango huo huku Kocha wa Fluminense, Fernando Diniz akiendelea kuwa kocha wa muda kwa miezi 12 ijayo huku akiendelea katika mechi za awali kufuzu Kombe la Dunia.