LONDON, England
MCHEZAJI nyota namba moja duniani katika tenisi, Carlos Alcaraz, ametinga hatua ya 16 Bora ya michuano ya Wimbledon baada ya kutandika Nicolas Jarry ambaye ni wa 25 kwa ubora wa viwango.
Nyota huyo, 20, alishinda kwa seti nne 6-3 6-7 (6-8) 6-3 7-5 uwanjani Centre Court katika mchezo wa raundi ya tatu ambao ulichukua kama saa 4.
Alcaraz atacheza na mshindi wa pili wa michuano hiyo 2021, Matteo Berrettini wa Italia ambaye alimtandikaMjerumani, Alexander Zverev.
Katika mchezo mwingine, Daniil Medvedev ambaye ni watatu kwa ubora, alimtandika Marton Fucsovics.