Try Again: Tutashusha ‘chuma’ kingine

Na Asha Kigundula

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, amesema yeye na Rais wa Heshima, Mohamed Dewji ‘MO Dewji’, wamesajili mchezaji mkubwa kutoka klabu kubwa barani Afrika na muda si mrefu atatambulishwa.

Akizungumza kabla ya hafla maalumu ya ufunguzi wa kadi maalum za uanachama wa klabu hiyo kwa kushirikiana na Benki ya CRDB katika Viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam le, Try Again amesema msimu huu wamefanya usajili mkubwa ambao wana uhakika wa kufanya vizuri katika michuano yote watakayoshiriki.

“Mimi na Mohamed Dewji tumefanya usajili mkubwa wa mchezaji mkubwa wa kutoka kwenye klabu kubwa, lengo ni kuhakikisha tunafanikisha malengo tulijiwekea ya kufanya vizuri kitaifa na kimataifa,”amesema Try Again.

Amesema kuwa wapinzani wao hawataamini macho yao kwa msimu mpya wa 2023/24 kutokana maandalizi wanayofanya na wachezaji waliosajili.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdul Majid Nsekela, amesema wameanzisha Simba Akaunti maalum kwa mashabiki wa timu hiyo ni pamoja na kadi maalum za watoto na wanawake kupitia timu ya Simba Queens.

Amesema kupitia kadi ya Simba, shabiki wa timu hiyo atapata bima ya sh. milioni 2, ambapo ufunguzi wa kadi hiyo ni sh. 2000 na zoezi hilo limefunguliwa kwa kila mwanachama anayetaka kuwa na kadi hiyo.

Pia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula, ameongeza ushirikiano wao na CRDB utakuwa na kadi za aina tatu ambazo ni kadi kwa watoto chini ya miaka 18, kadi ya mashabiki wa kawaida na kati za Platinum.

Katika hafla hiyo, imepambwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kama Menja Kunta na Tunda Man, pamoja na mashabiki mbalimbali wa timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *