LAS VEGAS, Marekani
PROMOTA Eddie Hearn, amesema Anthony Joshua na Deontay Wilder, karibu watakubaliana kuzichapa nchini Saudi Arabia.
Wawakilishi kutoka Mashariki ya Mbali, walisafiri kwa ndege kwenda London wiki iliyopita kufanya mazungumzo na Hearn kwa pambano hilo kubwa lililopangwa kufanyika kati ya Desemba au Januari.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendelea tena wiki hii kwa mpango wa pambano hilo la Joshua, 33, na Wilder, 37.
Hearn alizungumza na Boxing News: “Ni wazi tutafanya kikao na watu wa Saudi Ijumaa, Alhamisi na makubaliano yanaenda kufikiwa kwa kila kitu kwenda vizuri tukimalizia mazungumzo ya mwisho.
“Tulikutana nao tena Jumatatu. Nafikiri tupo katika nafasi nzuri lakini tunataka pambano liwe Agosti 12, ni muhimu kwa maendeleo ya kuwa na kasi yake anayofanya na huo ndio mpango bado.”
Hearn pia amekuwa akifanya udalali wa kurudi mara moja kwa AJ katika tarehe iliyopangwa ya Agosti 12.
Pia Dillian Whyte, aliyepigwa na Joshua mwaka 2015, amesaini mkataba wa pambano hilo kwenye Uwanja wa O2 Arena.
Hearn hapo awali aliweka wazi wiki hii kuwa ya mwisho kwa Whyte, 35, kukubaliana na masharti, ili kufungua njia ya kutangaza rasmi.
“Lakini kuna uwezekano mkubwa Jumatatu au Jumanne inawezekana tukatangaza.”
Ciao…