Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi awashukuru Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kwa kukubali kukaa pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM ili kuendeleza dhamira ya kushirikiana na kuimarisha Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Ameyasema hayo leo alipozindua Kamati ya maridhiano kati ya CCM na ACT Wazalendo Ikulu, Zanzibar.

Aidha Dk.Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kuridhia, kufanya vikao na Viongozi wa vyama vya siasa na kusikiliza maoni yao ambayo ameendelea kuyafanyia kazi na kutekeleza kwa vitendo azma ya kuleta maridhiano ya kisiasa ikiwemo kuunda Kikosi Kazi kilichopitia ripoti ya mkutano wa Baraza la vyama vya siasa na kutoa mapendekezo.

Vilevile kwa kuimarisha uhuru wa kisiasa na kidemokrasia kwa kuruhusu tena mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kuanzisha mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk.Mwinyi amesema hotuba yake aliyoitoa Mwezi Novemba Mwaka 2020 wakati anazindua Baraza la Wawakilishi kuwa dhamira yake ni kuwaunganisha wananchi wote wa Zanzibar kuwa wamoja, bila kujali rangi, asili, imani za dini au itikadi za kisiasa.

Halfa hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman na ujumbe wake pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais, Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Mhe.Hemed Suleiman Abdullah na ujumbe wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *