Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mapokezi ya ndege mpya ya mizigo ya Tanzania aina ya Boeing 767-300 itakayowasili nchini wiki hii Jumamosi Juni 03, 2023 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL), ndege hiyo mpya iliyotengenezwa nchini Marekani ina uwezo wa kubeba Tani 54 kwa safari moja hivyo kuondoa adha kwa wafanyabiashara waliokuwa wanasafirisha mizigo kuja ndani ya nchi.