Jana kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na USM Alger kulitokea vurugu za mashabiki kuvunja mageti ya uwanja na kuingia uwanjani ambapo katika kurupushani hizo, kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu mtu mmoja alifariki na wengine 30 kupata majeraha.
Klabu ya Yanga iliyokuwa mwenyeji wa mchezo huo mkubwa Barani Afrika imeungana na wapinzani wao Simba pamoja na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kutoa pole kwa kifo hicho na majeruhi wote.