Lifti yaporomoka ghorofani Dar na kujeruhi. Chalamila atia neno.

Lifti katika jengo la Millenium Tower lililopo Makumbusho Jijini Dar es Salaam limeporomoka na kujeruhi watu 7 waliokuwa wakiitumia leo Jumatano Mei 24, 2023.

Akizungumza na wanahabari, Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la zimamoto Patrick Afande amesema chanzo cha kuporomoka kwa lifti hiyo ni kushindwa kuhimili uzito mkubwa kinyume na kiwango chake ambapo ilibeba zaidi ya watu 10 ambao ni wengi ukilinganisha na uwezo wa lifti hiyo.

Lifti hiyo imeporomoka ghorofa ya 10 na kujeruhi watu 7 ambao katika majeruhi wote sasa wamepelekwa katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila mapema mchana huu alifika kwenye jengo hilo kujionea ajali hiyo ambapo amesisitiza wamiliki wote wa majengo katika Jiji la Dar es Salaam kujiridhisha na umadhubuti wa lifti katika majengo yao huku akisema uchunguzi unaendelea kuhusu hitilafu ya lifti hiyo na kwamba kama mmiliki wa jengo hilo alipewa taarifa (notisi) ya kukarabati lifti yake na hakufanya hivyo basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *