
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Patrobas Katambi, amewahakikishia wafanyabiashara nchini kuwa, serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji wa viwanda na biashara kulinda soko la ushindani.
Katambi ametoa ahadi hiyo jana Desemba 5,2025 jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kufunga Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani yaliyoandaliwa na Tume ya Ushindani (FCC).
Katambi ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amehimiza matumizi ya Akili Mnemba katika kuboresha ushindani na kulinda maslahi ya walaji wa bidhaa mbalimbali.
“Kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni ‘Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani’, inalingana na dhana ya kimataifa ya ‘Artificial Intelligence (AI), Consumers and Competition Policy’, ni vyema teknolojia hii tunaitumia vyema itusaidie kupiga hatua kwa maslahi mapata ya Taifa letu,” amesisitiza.

Amesisitiza kuwa kuwa teknolojia ya Akili Mnemba ni zana muhimu katika kudumisha ushindani wa haki, kulinda maslahi ya walaji, na kuongeza uwazi katika soko.
Amesema serikali imejipanga kuwa daraja na si ukuta, kuhakikisha sera zinazolinda walaji na wafanyabiashara zinatekelezwa ipasavyo.
“Hususan katika matumizi ya TEHAMA na AI. Pia kuhakikisha serikali inaweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwenye biashara na kulinda maslahi ya mtumiaji wa bidhaa,” amesisitiza.
Awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, akizungumza kwenye mkutano huo, ameeleza namna FCC ilivyoadhimisha Siku ya Ushindani Duniani kwa kuyafikia makundi muhimu ikiwamo kutoa elimu kwa jamii, wanahabari, wanasheria, wanafunzi kuhusu haki zao.
“Maadhimisho haya tulianza kwa kwa shughuli za kijamii, ikiwamo utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu haki zao, umuhimu wa uwazi katika masoko na namna ya kuepuka vitendo vinavyokandamiza ushindani katika soko,” amesisitiza.
Amesema pia wanadhibiti muungano wa kampuni unaofifisha ushindani ikiwamo kuhakikisha kampuni zinatoa huduma au kuzalisha mali zinatakiwa au zinahitajika kuitaarifu FCC kuhusiana na lengo la kuunganisha shughuli zao za kibiashara au kampuni moja kununua hisa za kampuni nyingine au kuinunua kampuni nyingine ili kuondoa ukiritimba unaoweza kutokea baada ya muungano huo. Kizingiti kilichowekwa na
Aidha, Ngasongwa amesema FCC kwa sasa thamani ya pamoja au mauzo ya mwaka yanayofikia Sh. bilioni 3.5 na kampuni ambazo zinapanga kuunganisha shughuli zao za kibiashara ambazo hazifikii thamani hiyo, zinaweza kufanya hivyo bila kulazimika kuitaarifu FCC.

“Tume ya Ushindani (FCC) itaadhimisha kitaifa Siku ya Ushindani Duniani mwaka 2025, Desemba 5, katika Hotel ya King Jada iliyopo Morrocco Square jjini Dar es Salaam ambapo Kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Artificial Intelligence (AI), Consumers and Competition Policy iliyotafsiriwa kuwa “Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani”.”
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT), Jaji Rose Ebrahim, amewataka wananchi na wafanyabiashara kutoa taarifa za vitendo viovu visivyo vya haki katika soko.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani, Dkt. Aggrey Mlimuka, amesema uhusiano kati ya AI na ulinzi wa walaji ni kuhakikisha uwazi na ufanisi katika biashara.

