
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
VIJANA wa Afrika wamepaza sauti katika maadhimisho ya Kanda ya Afrika ya wiki ya Kimataifa ya uelewa wa kudhibiti usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa (WAAW2025) iliyoanza mapema Desemba 2-5 2025, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Katika kongamano hilo la Saba Afrika likianza na mada maalum ya (Youth in AMR action) Vijana mbalimbali wameshiriki ikiwamo nchi za Nigeria, Kenya, Tanzania na nchini zingine ambao pia walipata kuhudhuria kupitia mtandao (Live).
Mwakilishi wa Umoja wa vijana kutoka Afya Moja na Shirika la AfricaCDC kwa Tanzania, Yuda Sule Paschal ameelekeza kilio chake kwa watunga sera ambao wamekuja wakijifungia wenyewe bila kuwashirikiaha Vijana ilikupata usahihi wa mahitaji katika mapambano ya kukabiliana na usugu wa Vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa (UVIDA),
Yuda amesema kuwa, vijana wanatakiwa kupata uelewa mpana juu ya UVIDA hivyo wafadhili, watunga sera na wadhamini wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kusaidia kundi hilo Tanzania na Afrika kwa ujumla.
“Serikali na wadau wajitokeze kusaidia miradi ya Vijana kwa mahitaji ya kifedha na rasilimali ili Vijana waeze kutimiza malengo yao katika kufikisha ujumbe na kuwa fikia vijana wengi zaidi.
Yuda ameongeza kuwa, katika changamoto pia ni nyingi kwa vijana wengi wa Afrika:
“Mimi nafanya kazi kupitia mashirika mbalimbali, ikiwamo Afya Moja, Afrika CDC, sisi Vijana tunapata changamoto ni kutojumlishwa kwenye kutunga sera na sehemu ya kutunga bajeti hali ambayo uwakilishi wa vijana unakuwa chini.
Lakini pia katika upatikanaji wa rasilimali, ikiwamo fedha, rasilimali vitu, changamoto ya lugha, kwani lazima ubadilishe lugha ya kitaalamu ili kukidhi matakwa husika, kufika maeneo ya mbali zaidi kama huna bajeti hufiki huko kwa vijana,
Hata hivyo, Yuda amebainisha kuwa, kama vijana wanaamini kilio chao kitapokelewa na kitafanyiwa kazi.
“Kila nchi wamewasilisha Mawasilisho ya Nchi zao ikiwemo changamoto na namna ya kuyafanyia kazi na sisi Tanzania pia tunaamini viongozi watayapokea.” amesema Yuda Paschal.
Aidha, vijana wengine waliweza kuwasilisha mada ikiwemo mashirika ya DRASA na Triple A kutoka Nigeria, REACT AFRICA kutoka Kenya na Yuda Africa CDC mwakilishi wa Tanzania.




