
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya CCM, Anthony Mavunde, ameendelea na awamu ya kwanza ya kampeni yake ya mtaa kwa mtaa, kwa kila kata kuzungumza na makundi mbalimbali katika maeneo husika.
Mavunde ameendelea na ziara yake Kata ya Ihumwa na kutembelea na kuzungumza na wananchi wa Mitaa ya Chang’ombe, Chilwana, Ilolo na Ihumwa.
Mavunde pia ametumia fursa hiyo kuwaombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Samia Suuhu Hassan na Mgombea Udiwani wa kata ya Ihumwa, Edward Magawa na madiwani wengine wa jimbo hilo.






