
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema azma ya Serikali yake ni kuanzisha mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia madini ya urani.
Dkt Samia ameyasema hayo, leo Jumamosi Septemba 22, 2025 alipozungumza na wananchi wa Songea Mjini mkoani Ruvuma, katika mkutano wake wa kampeni za urais.
Amesema azma ya Serikali yake ni kuhakikisha madini ya urani yanachimbwa, yanachakatwa na kusafirishwa yakiwa tayari yameongezwa thamani.
Sambamba na hilo, ameahidi kuanzisha mtambo wa kuzalisha umeme wa madini hayo, kwa kuwa nishati yake inakubalika kuwa safi.




