Na Sarah Moses, Dodoma.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mohamed Abood Mohamed amesema viongozi wote ambao wanasifa za migogoro na tabia zisizoridhisha hawatakiwi kwenye chama na hawatowavumilia.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 1,2025 jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa kupigiwa kura za mapendekezo na wajumbe kwa nafasi za Ubunge na uwakilishi w za jumuiya hiyo.
Amesema kwenye Chama hicho wanatakiwa watu safi, kiongozi anayetetea maslahi ya Taifa, mtenda haki, mchapakazi, asiyemwoga na anayejua wajibu na mipaka yake katika kazi.
“Vijana ndio Dira ya kusimamia misingi ya uhai wa Taifa na kusimamia maendeleo na mafanikio ya nchi, kila litakalitokea hapa likiwa na sura nzuri tutakuwa tumetoa sura ya uzuri wa Chama na nchi kwa ujumla” amesema.
“Likitokea kosa lolote tutakuwa tumeharibu sura ya Chama chetu, hapa tunafanya jambo kubwa kwa maslahi ya Chama chetu, hivyo lazima tufanye kazi hii kwa uadilifu na kufuata taratibu zote,”.
Amesema kazi hiyo inapaswa kufanywa kwa uadilifu mkubwa ili kila aliyepo humo aridhike na matokeo yatakayotangazwa.
“Wagombea tunao 58 wamekubalika na Chama ndio maana wameletwa kwetu ili tuwapigie kura za mapendekezo na baadaye Chama kitafanya maamuzi ya mwisho.
Katika hatua nyingine Mjumbe huyo akizungumzia kuhusu rushwa amesema rushwa ni adui wa haki hivyo lazima kwanza wachague viongozi wasiopenda rushwa hairuhusiwi atakayetoa na kupokea ndio atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye msafara.
“Wako watu inasemekana wanapanga matokeo hilo halitatokea hapa, wapo wenye nia ya kutoa rushwa na wengine wameanza kujitokeza watakuwa wamejiharibia safari yao,”amesema.
Kwaupande wake Katibu Mkuu wa UVCCM,Jokate Mwegelo amesema kuwa siasa siyo vita bali ni mchakato wa demokrasia hivyo watakaochaguliwa waungwe mkono kwa maslahi ya Jumuiya.
Amesema mara baada ya uchaguzi kumalizika wavunje makundi ili kuijenga jumuiya yenye umoja na mshikamano.
Amesema waasisi wa Taifa hili wameishi katika misingi ya umoja na mshikamano jambo ambalo vijana wanapaswa kulienzi na kuliishi.
“Sisi vijana tunapaswa kuishi kwenye misingi hiyo hata baada ya kumalizika kwa uchaguzi,tunapaswa kuvunja makundi na kurudi mezani pamoja” amesema.
Mwisho