
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimesema wataanza kutumia nembo maaalum(QR Code) kuweza kuhakiki na kutambua taarifa rasmi inayotolewa na chama hicho.
Lengo la kutumia nembo hiyo ni kuzuia na kudhibiti uzushi, unaotolewa na watu wenye malengo ovu ya kupotosha na kuzua tafrani kwenye chama hicho.
Katibu wa Halmashauri ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, ameyasema hayo leo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kufuatia upotoshaji na taarifa za uongozo zinazotoka kwa umma zikionesha zimetoka CCM.
“Uhakiki na uthibitisho huo unaweza kufanyika kwa ‘ku-scan` nembo hiyo, ambapo mara moja itakupeleka kwenye taarifa halisi iliyopo kwenye vyanzo rasmi vya Chama Cha Mapinduzi, ikiwa ni pamoja na tovuti na kurasa za mitandao ya kijamii.
“Taarifa yoyote ya uongo, ambayo watu wenye malengo ovu wanakuwa wameitengeneza kwa ajili ya kuzua tafrani na kupotosha jamii, msomaji `aki-scan, hawezi kupelekwa, wala hawezi kuikuta, kwenye vyanzo rasmi vya chama, iwe tovuti au kurasa za mitandao ya kijamii ya CCM,”amesema.
Makalla ametoa mfano mzuri ni taarifa iliyotengenezwa na kuzushwa Juzi, ambayo ilikanushwa, msomaji ‘aki-scan` atapelekwa kwenye chanzo rasmi cha chama, lakini atakuta kichwa cha habari kisemacho ‘CCM yatoa rambirambi kwa ajali gari iwambi, Mbeya.’ Jambo ambalo linadhihirisha ilikuwa taarifa ya uongo.
“Chama Cha Mapinduzi kimetoa ufafanuzi huu ili kusaidia mtu yeyote akiamua kujiridisha iwapo taarifa anayoisoma imetolewa rasmi na CCM, anaweza kufanya hivyo kwa ‘ku-scan` nembo hiyo (QR Code) na kupata uhakika. Lakini pia Chama kinapenda kuwaepusha Watanzania na walaji wote wa habari dhidi ya taarifa au habari za uongo,”amesema.

ReplyForwardAdd reaction |