Prof. Mkumbo azitaka ilani za vyama vya siasa kuzingatia Dira 2050

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, ametoa rai kwa vyama vya siasa nchini kuzingatia Dira 2050 wanapotoa ilani zao.

Akizungumza leo Julai 8,2025 jijini Dar es Salaam mbele ya Wahariri na Waandishi wa Habari ,Prof. Mkumbo, amesema kuwa mchakato wa Dira 2050 imehusisha Watanzania wa makundi mbalimbali na miongoni kupitia vyama vya siasa.

“Vyama vya siasa 19 vimeshiriki kikamalifu,vyama vikubwa na vidogo vyote vimepata nafasi.Tulimuomba Msajili wa vyama vya siasa atuaandalie mkutano na vyama vya siasa wametoa maoni yao.

“Tumekubaliana kwenda safari moja ya Dira 2050 ya Tanzania Tuitakayo . Hivyo wanasiasa hatutabishana kuhusu dira ya maendeleo ila watapishana wanatumia usafiri gani kuifikia hiyo dira.

“Vyama vya siasa wamekubaliana kuweka Ilani inayoakisi  Dira 2050 na hata ccm Ilani yetu tumezingatia dira hiyo Hivyo  tunatarajia na vyama vingine vya siasa Ilani zao zitaangalia dira 2050.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *