Mkurugenzi TASAC atoa wito wananchi kusoma sekta ya usafiri majini

Na Salha Mohamed

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mohamed Salum, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa kusoma sekta ya usafiri majini.

Hatua hiyo imefika baada ya sekta hiyo kuwa na uhaba mkubwa wa mabaharia kutokana na uchache wa watu.

Hayo ameyasema leo Julai 7, mwaka huu wakati alipotembelea Banda la Wakala huo kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.

Aidha amesema vijana wengi wamekuwa wakisomea sekta zingine na kuacha Sekta ya Bahari ambayo amedai ina fursa nyingi za ajira na kwamba nakuwashauri wazazi na walezi kuwahamasisha watoto wao kusomea sekta ya bahari ikiwemo ubaharia.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mohamed Salum, akisalimiana na wafanyakazi wakati akiingia katika banda hilo

“TASAC imeshiriki maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara kwa lengo kutoa elimu juu ya majukumu ya Wakala huu ikiwemo kudhibiti usafiri majini pamoja na kuchagiza sekta ya usafiri Majini.

“Ukitembelea Banda letu utajua fursa zinazopatikana ikiwemo mfuko wa mafunzo ya Sekta ya Bahari,pia kwa upande wa wanawake wanapata fursa ya kusomea sekta ya Bahari, “amesema.

Amesema Wakala huo umekua ukisajili vyombo vya majini nakuvipa cheti cha ubora kwa ajili ya kufanya shughuli zake majini, ikiwa lengo ni kudhibiti sekta ya usafiri Majini.

Ameongeza kupitia wataalamu wake imekua ikifanya ukaguzi wa Meli za kimataifa zinazoingia nchini,pamoja na uwanda mzima wa Bahari ikiwemo kutoa taarifa ya uokoaji,hali ya hewa na taarifa kwa wavuvi ili kuweza kuchukua tahadhari,nakuhakikisha Bahari inabaki safi.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa TASAC ameendelea kusema kwamba Wakala huo umekua ukisimamia usalama wa bandari, kutoa leseni za bandari, kusimamia shughuli zote za ujenzi wa bandari.

Amewashukuru wadau kutembelea Banda la TASAC nakutoa wito kwa wasiofika kupita ili kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu shirika hilo pamoja na kujua fursa zinazopatikana katika sekta ya uchukuzi kwa njia ya maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *