Wateja waliobahatika wajishindia mil. 12.5/- droo kubwa ya KFC, Pizza Hut na Hisense

Na Mwandishi Wetu

WATEJA wawili waliobahatika, wamejinyakulia shilingi milioni 12.5 kila mmoja baada ya kushinda katika droo maalum iliyoratibiwa na KFC na Pizza Hut kwa ushirikiano na Hisense ikiwa ni chapa maarufu ya vifaa vya kielektroniki duniani.

Washindi hao, waliotambulika kwa majina ya Habiba Ali (kutoka KFC) na Alpha Isack (kutoka Pizza Hut), wamechaguliwa kupitia kampeni inayoendelea ya promosheni iliyolenga kuthamini uaminifu wa wateja.

Promosheni hiyo iliwapa nafasi wateja wote waliokuwa wakinunua bidhaa katika matawi ya KFC na Pizza Hut kote nchini kushiriki katika droo hiyo kwa urahisi.

Washindi wa zawadi kuu walitangazwa wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofana iliyofanyika katika Duka Kuu la Hisense lililopo Mlimani City, ikimaanisha uzinduzi rasmi wa ushirikiano mpya na wenye nguvu kati ya Hisense, KFC na Pizza Hut.

Kila chapa, inayotambulika kwa ubunifu, ubora na ushirikiano thabiti na wateja wake, imeungana katika ushirikiano wa kimkakati unaoleta msisimko mkubwa nchini kote.

Wateja wawili wenye bahati, Habiba Ali (kushoto) na Alpha Isack, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda droo ya wateja iliyoandaliwa na KFC na Pizza Hut kwa kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya vifaa vya kielektroniki, Hisense. Kila mmoja wao alizawadiwa vocha ya manunuzi yenye thamani ya shilingi milioni 12.5.

Kampeni hiyo haikulenga tu kutoa zawadi za kuvutia, bali pia kuimarisha uhusiano kati ya chapa hizo na wateja wao kupitia matukio ya kukumbukwa na yenye furaha.

“Tuna furaha kubwa kusherehekea na kuwazawadia wateja wetu kwa njia ya kipekee kama hii,” amesema Lyse Mosha ambaye ni Meneja Masoko wa KFC.

“Kampeni hii inaonyesha dhamira yetu ya kuunda matukio ya kukumbukwa huku tukithamini uaminifu wa wateja wetu.”

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo, Kalbe Husein ambaye ni Mwakilishi wa Hisense Tanzania, amesema: “Ushirikiano huu unazidi bidhaa, unahusu kuunda uzoefu wa pamoja. Kwa kuungana na KFC na Pizza Hut, tunatoa zaidi ya ubunifu na chakula bora, tunaleta msisimko, tunathamini uaminifu wa wateja na kuleta nyakati zisizosahaulika kwao.”

Wateja pia walipata fursa ya kujionea teknolojia mpya kutoka katika bidhaa za kielektroniki na vifaa vya nyumbani vya Hisense, sambamba na kufurahia ladha maarufu za vyakula kutoka KFC na Pizza Hut.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *