Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu wapungua.

Sarah Moses,Dodoma.

WIZARA ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Magereza imefanikiwa kuondoa changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu magerezani ambapo umepungua kutoka 33,7640 mwaka 2020/21 hadi kufikia 27,088 mwezi Aprili 2025.

Hayo ameyasema leo Bungeni Mei 26, 2025, Waziri wa wizara hiyo Innocent Bashungwa wakati alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo amesema kuwa juhudi hizo zimetokana na Serikali ya awamu ya sita.

“Hii inaonesha wafungwa na mahabusu 6,676 wamepungua magerezani, sawa na asilimia 20 ya uwezo wa Hata hivyo, kupitia juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita msongamano wa wafungwa na mahabusu magerezani umepungua kutoka 33,7640 mwaka 2020/21 hadi kufikia 27,088 mwezi Aprili 2052 ya uwezo wa kisheria wa kuhifadhi wafungwa na mahabusu 29,902. 20”amesema Waziri Bashungwa

Pamoja na hayo amesema Wizara kupitia Jeshi la Magereza imefanikiwa kutumia nishati safi katika magereza yote 129 kwa ajili ya kupikia chakula cha wafungwa na mahabusu magerezani,nakuema kuwa  utekelezaji huu ni sawa na asilimia 100 ya lengo ya kupeleka nishati safi kwa magereza yote nchini.

“Namshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa maelekezo yake 15 juu ya matumizi ya nishati safi ambayo yamewezesha Jeshi la Magereza kupata mafaniko haya”amesema.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *