TAMISA YATAKIWA KUDHIBITI WANACHAMA WAKE KUBORESHA HUDUMA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WIZARA ya Madini, imekitaka Chama cha Watoa Huduma za Sekta ya Madini nchini (TAMISA) kuwadhibiti wanachama wake ili kuondoa ubabaifu kwenye utoaji wa huduma.

Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mhandisi Yahaya Samamba, wakati akizindua Kamati ya Masoko na Mawasiliano ya Watoa Huduma katika Sekta ya Madini (TAMISA).

Amesema kuwa na nidhani ya utendaji kutawasaidia wao kuaminika na kupewa umiliki wa migodi na kuongeza ushiriki wa wazawa katika sekta ya madini.Samamba alisema serikali inazo taarifa za baadhi ya watoa huduma katika sekta ya madini ambao si waaminifu na wamekuwa wakileta ujanja, kucheza na kusambaza bidhaa ambazo hazina ubora.

Ametoa ushauri kuwa waifanye TAMISA kuwa na wakali kama ilivyo Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) ambayo imekuwa ikiwashughulikia wanachama wake wanaoharibu kazi.

“Kuweni kama ERB Mhandisi akicheza ERB wanamuwajibisha, jitahidini muwe na mfumo huu, mkifanikiwa mtakuwa watoa huduma wenye nidhamu wasiowaangusha. Hili ili liweze kufanyika ni kuwa na ushirikiano na sisi kama wizara tutawapa kwa asilimia 100,” amesema.

Amesema ni vyema pia wahakikishe wanakuwa na wanachama hai ambao watapatikana kwa kuhakikisha wote wanafuata taratibu zinazotakiwa kabla ya mtu kusajiliwakusajiliwa.

Naye Mwenyekiti wa TAMISA, Peter Kumalila, amesema lengo ni kusaidia wanachama kukuza biashara kuwajengea uwezo ili washindane katika sekta hiyo.

Amesema hatua hiyo inaenda sambamba na kutetea haki za wanachama pale panaAAAApotakiwa.Hata hivyo, Kumalila alisema mara zote watahakikisha wanafanya mchujo wa kina ili wanachama waaminike na waepuke kuharibu kazi wanazopata mgodinHiyo ni kutokana na kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wadau juu ya baadhi ya wazawa wanaopewa kazi na kuzembea au kufanya kazi kwa viwango visivyokubalika.

“Hili jambo tumelipokea kwa uzito mkubwa sana, tumejilanda kuhakikisha TAMISA inafanya tathmini ya kina kabla ya mwananchama kupewa kazi ili kuimarisha uaminifu na kuepusha mgogoro,” amesema.

Ametumia nafasi hiyo kuiomba serikali kushughulikia changamoto ya uwapo wa wimbi la wageni kupewa kazi ambazo wazawa wanaweza kuzifanya.

“Tunaomba serikali iingilie kati kuhakikisha haki inatendeka na tunashauri suala la ubia lizingatie sheria na kanuni na ushiriki wa wazawa,” amesema Kumalila.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Masoko na Mawasiliano iliyozinduliwa, Dkt. Sebastian Ndege, amesema kwa sasa Tanzania ina madini aina mbalimbali na kampuni zimekuwa zikiwekeza hivyo ni wakati wa Watanzania kuimarisha ushiriki wao katika uchumi wa madini.Alisema wanafahamu kuwa wanayo haki ya kushiriki katika kutoa huduna lakini pia wanao wajibu wa kuhakikisha wanatoa huduma sahihi kwa wakati sahihi na weledi.

“Sisi kama TAMISA kazi yetu itakuwa ni kusimamia wanachama wetu kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa tunafuata maadili ya utoaji hufuma ili tuweze kuaminika na hili tutalisimamia kwa nguvu zetu zote,” amesema Dkt. Ndege.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *