Serikali kutumia Tril. 1.18/- kujenga miundombinu ya barabara za wilaya

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Katika mwaka wa fedha 2025/26, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imepanga kutumia Sh. trilioni 1.18 kwaajili ya ujenzi, matengenezo, ukarabati wa miundombinu ya barabara na usafiri na usafirishaji wa vijijini na mijini.

Kati ya fedha hizo Sh. bilioni 257.03 ni za Mfuko wa Barabara, Sh. bilioni 127.50 Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali, Sh. bilioni 325.77 ni za tozo ya mafuta ya petroli na dizeli ya Sh. 100 kwa lita na Sh. bilioni 423.79 ni fedha za nje.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 jijini Dodoma.

Amesema kupitia Mfuko wa Barabara, fedha hizo zitaenda kutekeleza matengenezo na ukarabati wa barabara za wilaya zenye urefu wa Kilomita 23,105.78, box kalavati 23, mistari ya kalavati 1,647, Drift 2, na mifereji ya maji ya mvua mita 73,405, barabara za lami kilometa 17, barabara za changarawe Kilometa 108.8 na madaraja 2.

Aidha, ujenzi wa Kilometa 91.97 kwa kiwango cha lami, Kilometa 2,621.40 za changarawe, madaraja 85, box kalavati 91, mitaro ya maji ya mvua mita 10,989 drifti tano (5), mistari ya kalavati 666 na taa za barabarani 345 zitatekelezwa kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

Aliongeza kuwa kupitia tozo ya mafuta ya petroli na dizeli ya Sh. 100 kwa lita, fedha hizo zitatekeleza ujenzi wa Kilomita 252.42 kwa kiwango cha lami, Kilomita 6,939.41 za changarawe, madaraja 51, box kalavati 336, mistari ya kalavati 1,719, Drift 2, na mifereji ya maji ya mvua mita 63,836.

Mchengerwa amesema ujenzi wa barabara za lami Kilomita 147.50, ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua mita 24,600, ujenzi wa masoko 9, ujenzi wa stendi kuu za mabasi na stendi ndogo 2 pamoja na ujenzi wa maghala 2 ya kuhifadhia mazao kwenye miji 12 ya Fungu la Kwanza la Mradi wa TACTIC unaendelea.

Pia kuanza kwa ujenzi kwenye Halmashauri za Miji 15 za Fungu la Pili la Mradi wa TACTIC pamoja na kukamilisha mchakato wa maandalizi ya Mradi wa TACTIC Fungu la Tatu katika Halmashauri za Miji 18.

Amesema ujenzi wa barabara Kilomita 33 kwa kiwango cha lami katika halmashauri za Wilaya za Iringa (Wenda-Mgama kilomita 19) na Mufindi (Mtili-Ifwagikilomita 14) unaendelea, pmoja na kuanza kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Kilomita 33 katika halmashauri za Wilaya za Handeni, Ruangwa na Mbogwe kupitia mradi wa RISE.Vilevile, uboreshaji wa Bonde la Msimbazi lenye Hekta 5.7, ujenzi wa karakana ya mabasi ya mwendo kasi katika eneo la Ubungo Maziwa, ujenzi wa tuta kilomita 6.7 katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi, ujenzi wa Bohari Mpya ya BRT eneo la Ubungo Maziwa, ujenzi wa miundombinu ya barabara awamu ya kwanza zenye jumla ya kilomita 132 katika Manispaa za Kinondoni,Ubungo, Temeke, Ilala na Kigamboni.

Pia, ujenzi wa miundombinu ya barabara awamu ya pili ya Mradi wa DMDP zenye urefu wa Kilomita 118 kiwango cha lami katika Manispaa za Kinondoni, Ubungo,Temeke, Ilala na Kigamboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *