TCB yazindua huduma mpya ya LIPA POPOTE

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua wa bidhaa ya LIPA POPOTE, suluhisho la malipo lililobuniwa ili kurahisisha miamala kwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) na wamiliki wa biashara.
Bidhaa hiyo mpya inawawezesha wateja wa Benki ya TCB kupokea malipo moja kwa moja kwenye akaunti zao za benki kupitia namba moja ya mfanyabiashara iitwayoLIPA POPOTE.


Ofisa Mkuu wa Huduma za Kidijitali na Ubunifu wa Benki ya TCB, Jesse Jackson, aliyaeleza hayo juzi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Amesema wenye akaunti ya benki hiyo, wataweza kulipia bidhaa na huduma kwa urahisi wakitumia namba maalum ya muuzaji (Till Number), hivyo kufanya miamala iwe rahisi zaidi kuliko hapo awali.

Amesema LIPA POPOTE imebuniwa kushughulikia hitaji la malipo ya kifedha linaloongezeka kwa
kasi nchini miongoni mwa wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) ambao ni uti mgongo wa uchumi wa taifa. Suluhisho hili linalenga kurahisisha mchakato ya malipo kwa wamiliki wa biashara, kuwawezesha kupokea malipo papo hapo na kwa usalama.
Bila kuhitaji gharama za usajili, huduma hii inapatikana kirahisi, ikiongeza wigo wa
ujumuishi wa kifedha kwa kuondoa vizuizi vya miamala ya kidijitali kwa biashara mbalimbali kote nchini.
“TCB tumekusudia kukuza ubunifu unaogusa maisha ya Watanzania.

Amesema LIPA POPOTE inadhihirisha dhamira yao ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs) kwa kutoa suluhisho bora kwa malipo rahisi na salama,” alisema Jacson.

“LIPA POPOTE ni zaidi ya njia ya malipo; ni hatua kuelekea uwezeshaji wa kiuchumi kwa
wafanyabiashara nchini, kuanzia mijini hadi jamii za vijijini. Lengo letu ni kuzifanya
huduma za kifedha ziwe salama, nafuu na zipatikane kwa watu wote,” alisisitiza Jackson.
“Kwa kuzindua suluhisho la kidijitali la malipo kama vile LIPA POPOTE, tunaboresha kikamilifu malengo ya Tanzania ya kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa wafanyabiashara, watu binafsi na jamii ambazo hazijafikiwa bado. Njia hii ya malipo inatarajiwa kubadilisha namna biashara ndogo zinavyofanya kazi na kurahisisha miamala ya kifedha,” amefafanua.

Naye Mkurugenzi wa Biashara kwa Wateja Wadogo na wa Kati, Lilian Mtali, amesema “Tunashuhudia mageuzi ya kidijitali yanayoendelea kuboresha uchumi wetu kila
kukicha, TCB inalenga kuwa mstari wa mbele katika kutoa masuluhisho ya kibenki yenye ubunifu na kuchochea ujumuishi wa kifedha kwa wote,” amesema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Adam Mihayo, amesema “LIPA POPOTE ni uthibitisho wa dhumuni letu la uwezeshaji uchumi na upatikanaji wa huduma za kifedha, ili kuwanufaisha Watanzania wote na huduma za kisasa za kibenki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *