TFRA yawataka wakulima kujisajili kupata mbolea ya ruzuku

Sarah Moses,Dodoma.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imewataka Wakulima kujisajili kwajili ya kupata mbolea ya Ruzuku ili kulima kilimo chenye tija kwao na kwa Taifa kwa kupata mazao mengi yenye ubora yanayohitajika katika soko.

Hayo ameyasema leo Agosti 7 jijini Dodoma kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Ndani TFRA Luis Kasera ambapo amesema ili kupata mafanikio katika kilimo  na kibiashara lazima kuzingatiwa kwa matumizi ya Mbolea .

Amesema lengo la Wakulima kujisajili ni kujua maeneo wakulima walipo na idadi yao ili kuhakikisha kiwango cha Mbolea kinachopelekwa katika maeneo hayo kinalingana na uhitaji.

Amesema kuwa mpaka sasa wamesajili wakulima milioni 4 na lengo nikuwasajili wakulima milioni 7 nchi nzima  kwamwaka 2024/205,

“Kwa wale ambao tumesajili kipindi cha  nyuma sasa tunaenda kuchukua picha zao,alama za vidole lengo nikujua  mkulima yupo wapi na ninani ili serikali inapomsaidia ijue itampata wapi”amesema.

“Tunawasihi wakulima wajitokeze kwa wingi kujisajili na watoe tarifa ambazo ni sasa ili waweze kusaidiwa kwa urahisi” amesema.

Amewataka wakulima kununua mbolea mapema sababu mbolea ipo yakutosha lakini pia itawasaidia kujua eneo gani linamapungufu ya mbolea ili waweze kupeleka.

“Kwasasa hivi tunatani zaidi ya laki tatu nchini ambapo zipo kwaajili ya kupandia na nyingine ni mbolea ya kukuzia”amesema.

Mwisho. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *