Na Sarah Moses, Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeweka mazingira wezeshi ya kuweza kuhamasisha uwekezaji wa ndani ili angalau inapofikia mwaka 2030 tuweze kupunguza kiasi kikubwa cha uagizaji wa Mbolea kutoka nje.
Hayo ameyasema Agosti 5,2024 Meneja wa Usajili na Leseni wa mamlaka hiyo Mwaija Almas wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya nane nane ambayo yanafanyika Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema kuwa lengo la kufanya hivyo nikuokoa gharama kubwa ambayo serikali inaingia kwa ajili ya kusaidia kuagiza Mbolea kutoka nje kwa kutumia dola.
Amesema kuwa wanahamasisha uwekezaji wa uzalishaji wa Mbolea nchini kwani zaidi ya asilimia 90 ya Mbolea inayotumika nchini ni ile ambayo inaagizwa kutoka nje
Akizungumzia swala la ubora wa mbolea amesema kuwa mamlaka inafanya kaguzi za mara kwa mara katika maeneo ambazo zinauzwa.
“Tunafanya ukaguzi wa kushtukiza na ule ukaguzi wa kutangaza ambapo kule ndipo wanapojiridhisha iwapo Mbolea ilipooingia inaendelea kuwa na ubora uleule mpaka inapoenda kumfikia mkulima”amesema
“Tunazo ofisi za Kanda nne ambapo tumerahisisha utoaji wa huduma zetu kwa wadau, hivyo tunaofisi Kanda ya kuu kusini Mbeya, ukanda wa Kaskazini Arusha, Kanda ya ziwa Mwanza ,Kanda ya Kati Tabora na Kanda ya Mashariki Dar es Salaam na Dodoma pia wameanzisha ofisi hao mpya”
Hii yote ni katika kuhakikisha kwamba wadau wanawafikia kwa urahisi nakuongeza ufanisi katika huduma zao.
Kwaupande wake Meneja wa Ukaguzi wa Mbolea kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea TFRA DKt Ashery Kalala amesema kuwa jukumu lao ni kuhakikisha mkulima anapata Mbolea iliyokuwa na ubora .
” Na toa wito kwa wakulima wake wajifunze ambapo Tume Weka vipando ambavyo vinaonyesha mahali ambapo tumetumia Mbolea na ambapo hatujatumia Mbolea.
Mkulima akiitumia ipasavyo Mbolea anaweza kupata mavuno yaliyokuwa mazuri na mengi .
Hivyo basi tunamhimiza mkulima waweze kutumia Mbolea kwa usahihi kwani kwa kufanya hivyo inaondoa dhana ya kwamba Mbolea inaharibu udongo au mkulima kutumia Mbolea halali inaonekana kama mkulima hajatumia vizuri.
“Tunamhimiza mkulima apime udongo baada ya hapoatajua ni virutubisho gani ambavyo vimepungua kwenye udongo wake na baada ya kujua basi tunamshauri ni Mbolea gani atumie.
Mwisho.