PBPA yaeleza mafanikio mfumo uagizaji mafuta wa pamoja nchini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAKALA wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), umesema tangu kuanza kwa mfumo huo nchini mwaka 2015, muda wa meli kushusha mizigo umepungua kutoka siku 40 hadi 90 hadi kufikia chini ya siku tano.

Gharama za meli kusubiri kushusha mizigo kwa siku ni Dola 20,000 hadi 80,000 sawa na takribani Sh. milioni 53 hadi 211.

Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Bidhaa za Mafuta wa, Bruno Tarimo, ameyasema hayo jana mkoani Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).”

Baada ya mfumo kuanza meli inaweza kusubiri siku tatu hadi tano, hivyo utaona tumeokoa kwa kiasi kikubwa cha gharama za meli kusubiri na kusaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha,”amesema.

Amesema pia wameokoa upotevu wa mafuta kutoka asilimia 5 hadi kufikia chini asilimia 0.2.

Aidha, amesema kiwango cha nchi jirani zinazoagiza mafuta kupitia mfumo huo, kimeongezeka hadi kufikia asilimia 50 hadi 55.

Amesema kwasasa kiwango cha mafuta yanayotumiwa ndani na yale yanayoenda nchi jirani ni asilimia 50 kwa 50.

Amezitaja nchi zinazoagiza mafuta kwa mfumo huo kuwa ni Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na DR Congo.Kuhusu maonesho hayo ya Sabasaba, alisema wamefika kutoa elimu na kushawishi wafanyabishara na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kujiunga na mfumo huo ili kuagiza mafuta.

Amesema katika kuuratibu mfumo huo, wanapokea mahitaji kutoka kwa kampuni za mafuta, wanayachakata ili kupata kiwango kinachohitajika ili kuagiza kiwango kikubwa zaidi na kupata unafuu bei kwa mtumiaji wa mwisho.”Mafuta yanapoletwa kwa ufanisi huo kuna kuwa na unafuu mkubwa wa bei kwa mlaji wa mwisho” amesema Tarimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *