Na Sarah Moses, Dodoma.
KATIKA mwaka wa fedha 2024/25 Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,JInsia , Wanawake na Makundi Maalum imetaja vipaumbele 6 ikiwemo kuratibu afua za kukuza usawa wa kijinsia na kutokomeza vitendo vya ukatili.
Akizungumza leo Mei 17 Bungeni Waziri Dkt. Dorothy Gwajima wakati alipokuwa akiwasilisha Bungeni makadilio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema kipaumbele kingine ni kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa Ngazi ya Msingi.
Vipaumbele vingine ni uwezeshaji wanawake kiuchumi, upatikanaji wa haki, ulinzi na malezi chanya ya watoto, lakini pia kuratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za
msingi za ustawi wa jamii.
“Kutambua, kuratibu na kuendeleza Makundi Maalum wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo na kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika Taasisi na Vyuo vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na kuimarisha ushiriki na mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa” amesema.
Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, Wizara kwa mwaka 2024/25 imekadiria kutumia jumla ya kiasi cha Shilingi 67,905,259,000.
Mwisho.